Lijue Bunge la Afrika Mashariki na Jee Uchaguzi wa Wabunge wa CCM EALA Ulikuwa ni Uchaguzi Kweli Au Kiini Macho cha Uchaguzi?
Kwa Maslahi ya Taifa, inaendelea na makala elimishi za kuijua Jumuiya ya Afrika Mashariki, leo ni makala elimishi kuhusu kulijua Bunge la Afrika Mashariki, EALA na kiini macho cha uchaguzi wa Wabunge wa EALA wa Tanzania uliofanywa na Bunge letu!. Kilichofanyika kwenye uchaguzi wa EALA ndani ya Bunge letu, kunaacha maswali ya kujiuliza, hivi sisi Watanzania, “Do we real know what we need and what we want?!”, “if we do, we wouldn’t have let this joke of an election just passby!”.
Bunge letu lilipaswa kuletewa majina angalau mawili mawili kwa kila nafasi, halafu Bunge ndio lichague!. Kilichofanyika ni Bunge lilipelekewa majina ya kuchagua, uchaguzi uliofanyika ni wa mbunge mmoja tuu wa kutoka upinzani na kuthibisha majina 8 ya CCM!. Ili uchaguzi ufanyike, there must be choices to choose from, if there was no choices to choose from, huo haukuwa ni uchaguzi, ulikuwa ni kiini macho cha uchaguzi!.
Declaration of Interest
Kwa vile mimi nilishiriki mchakato wa uchaguzi huu ndani ya chama, nikashindwa kwa vigezo na kukubali kushindwa EALA: Waliopitishwa CCM, ni Kwa Haki!, Tulioachwa ni kwa Haki, Tumezidiwa Vigezo!. Thanks4 for Support, Nimekubali Matokeo Kiroho Safi! Kazi Iendelee! hivyo makala hii sio ya kutema nyongo ya kushindwa EALA bali hii ni makala elimishi kuelimisha umma kuhusu Bunge la Afrika Mashariki na kuwatendea haki Watanzania kwa kuwaonyesha matundu kwenye paa letu, hivyo kujua sisi Watanzania tunakwama wapi!.
leo tunamalizia mfululizo huu kwa SURA YA TISA: LIJUE BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI, JEE UCHAGUZI WA WABUNGE WA EALA ULIOFANYWA NA BUNGE LETU NI ULIKUWA UCHAGUZI KWELI AU NI KIINI MACHO CHA UCHAGUZI?.
Sura hii inajumuisha Ibara ya 48 mpaka Ibara ya 65. Bunge la Afrika Mashariki ni chombo kilichaonzishwa ili kutekeleza majukumu ya kutunga sheria za Jumuiya.
Idara ya 48 inahusu muundo wa Bunge
Bunge lina wajumbe 9 wa kuchaguliwa kutoka kila nchi na wajumbe 9 ambao wataingia kwa nyadhifu zao. Hawa ni mawaziri 7 wa wizara za Nje na Katibu Mkuu wa jumuiya na Mwanasheria Mkuu wa EAC.
Spika atakuwa na madaraka ya kumwalika mtu yeyote ambaye mchango wake utahitajika katika kujadili hoja yoyote iliyoletwa mbele ya Bunge.
Ibara ya 53 inahusu Spika wa Bunge.
Spika atachaguliwa kutokana na wajumbe wa Bunge. Cheo hiki kitashikwa kwa mzunguko kati ya Nchi Wanachama.
Ibara ya 49 inahusu Kazi za Bunge.
Mbali na wajibu wa kutunga sheria, Bunge la jumuiya litakuwa pia chombo cha kuendeleza mahusiano na mbunge ya kitaifa ya Nchi Wanachama kwa mambo yanayohusu jumuiya.
Bunge litakuwa na kazi ya kupitisha bajeti ya jumuiya. Kabla ya kupitisha bajeti, Bunge litaangalia na kutathmini ripoti za shughuli za Jumuiya. Kazi nyingine ya Bunge itakuwa ni kujadili mambo yote yanayohusu jumuiya na kupeleka mapendekezo kwenye Baraza la Mawaziri. Bunge litakuwa pia na kazi ya kupendekeza majina ya watu kwa ajili ya uteuzi wa nafasi za Katibu Mkuu na maofisa wengine wateule wa jumuiya.
Utaratibu wa Kutunga Sheria
Utungwaji wa sheria utaanza kwa kupelekwa muswada Bungeni. Ikiwa muswada utapitishwa na Bunge, Spika ataupeleka kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi ili wautolee kibali.
Wakuu wa Nchi wakiukubali, unakuwa sheria. Wakiukataa utahesabika kuwa umepitwa na wakati.
Kupitishwa kwa muswada wa sheria na Wakuu wa Nchi unataka makubaliano ya Wakuu wote wa Nchi. Iwapo Mkuu mmoja wa Nchi atakataa, bado muswada huo hauwezi kupita.
Kanuni za Bunge
Bunge lina uwezo wa kutengeneza kanuni zake. Sheria na kanuni hizi zaweza kuhusiana na uwezo, haki, kinga ya wabunge na utaratibu wa uendeshaji wa shughuli zake.
Miswada ya kupelekwa Bungeni inaweza kupendekezwa na mjumbe yeyote. Lakini miswada hii iwe inahusiana na shughuli za Jumuiya na sheria zilizoainishwa katika Mkataba wa Jumuiya, kufuati Tanzania kupeleka majanga EALA, Tangu kuundwa kwa EALA, hakuna mbunge yoyote wa Tanzania, amewahi kupeleka muswada wowote!, Wabunge wa Kenya na Uganda pekee ndio wanaotamba mule!, Tanzania ipo ipo tuu kama hatupo!, au ni tupo tuu kama watazamaji zaidi kuliko washiriki!.
Uchaguzi wa Wabunge
Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki watachaguliwa na Bunge la Taifa la kila Nchi Mwanachama. Kwa hiyo, kila anayetaka kugombea itabidi akapigiwe kura na Bunge la nchi yake. Kwa Tanzania sio kila anayetaka, bali kila aliyepitishwa na chama cha siasa!.
Kila nchi itachagua wabunge tisa, ambao watakuwa siyo wabunge katika bunge la nchi husika. Uteuzi wa wabunge hao utaangalia uwiano wa uwakilishi wa vyama mbalimbali vya siasa vilivyoweza kuingia katika bunge la nchi husika. Uteuzi utaangalia pia jinsia na uwakilishi mwingine muhimu katika kila Bunge la nchi, husika.
Sifa za kuchaguliwa kuwa Mbunge katika Bunge la Jumuiya:
Awe ni raia wa Nchi Mwanachama
Awe na sifa ya kuchaguliwa kuwa mbunge katika nchi yake kulingana na sheria na taratibu za nchi hiyo. Wabunge wa EALA sio wabunge wa vyama, wala Bunge la EALA sio Bunge la kupiga siasa. Nchi majirani zetu, hutangaza nafasi hizi, raia wake huziomba sio kupitia vyama, ili kupata watu wenye uwezo.
Kwa sisi Tanzania, nafasi hizi hugombewa kupitia vyama, mimi kama mwandishi wa habari, nimekuwa nikihudhuria vikao vya Bunge hili, ukiangalia jinsi wabunge wa nchi za wenzetu wanavyochangia mada na mijadala, ukilinganisha ni michango ya wabunge wa Tanzania, kusema ukweli, ukiondoa wabunge wawili watatu waliokuwa active mule, kiukweli kabisa katika EALA iliyopita, Tanzania tulipeleka majanga!.
Kufuatia Tanzania kupeleka majanga EALA iliyopita, fursa ya EALA ilipojitokeza tena, kwanza mimi nami kama Mtanzania mwingine yeyote, pia nilitupa karata yangu, lakini pia nikatoa ushauri wa jinsi ya kupata watu mahiri. Nilishauri
- Kwa waliokuwa wawakilishi wetu kwenye Bunge hilo ambao wanataka kuwania tena nafasi hizo ili kuendelea kwa awamu yao ya pili, waulizwe katika uwakilishi wao, ndani ya Bunge hilo kwa miaka 5 iliyopita, wamechangia nini na wamelisaidia nini taifa?. Hili ndio Swali la Mhe. Msukuma kwa mmoja wa wagombea.
- Wagombea wa set agenda za Tanzania kama nchi anazotaka kwenda kuzipigania kwenye EALA na kupewa dakika 5 za kujieleza kwa lugha ya Kiingereza safi kilicho nyooka!. Moja ya sababu za baadhi ya wawakilishi wetu kuwa mabubu kwenye mijadala ya kuchangia hoja za Bunge la EALA, ni mtiririko wa Lugha, yaani kuongea Kiingereza safi fluently.
Kufuatia Watanzania ‘kuwakataa wapinzani’ kwenye sanduku la kura, kupitia uchaguzi mkuu ‘huru’ na wa ‘haki’ kufuatia Tanzania kuendesha chaguzi zetu kwa mutatis mutandis, ni Mbunge mmoja tuu huku Bara toka upinzani ndio amechaguliwa, tena kuchaguliwa kwake ni kwa bahati tuu ya Mtende, kufuatia wananchi wa jimbo lake kumuadhibu mbunge wao, kwa kitendo chake cha kushabikia uvunjifu wa katiba katika ukomo wa uongozi, ile ya “Atake Asitake”, hivyo wananchi wakaamua kumpiga chini. Hivyo Bunge hili ni Bunge la chama kimoja predominantly, hivyo katika nafasi 9 za EALA, CCM ikapata nafasi 8 na upinzani nafasi 1.
Kiini Macho cha Uchaguzi Wa Wabunge wa EALA Bunge la Tanzania.
Sifa kuu ya kuchaguliwa EALA ni uraia wa nchi husika na (e) has proven experience or interest in consolidating and furthering the aims and the objectives of the Community.
Uchaguzi wa Wabunge
Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki watachaguliwa na Bunge la Taifa la kila Nchi Mwanachama. Kwa hiyo, kila anayetaka kugombea itabidi akapigiwe kura na Bunge la nchi yake.
Haki ya kila Mtanzania Kupiga Kura Ipo, ila Haki ya Kupigiwa Kura, Imeporwa!.
Kwa mujibu wa Ibara ya 5 ya Katiba ya JMT, kila Mtanzania aliyetimiza umri wa miaka 18, anaruhusiwa kupiga kura na kuchagua viongozi wake. Haki hii ya kila Mtanzania kuruhusiwa kupiga kura kuchagua viongozi wake, ilipaswa kwenda sambamba na kila Mtanzania kuwa na haki ya kupigiwa kura.