Kwa “nonsense” ya Sukari, Rais Samia anastahili pongezi. Je, tuishie kwenye “nonsense” ya Sukari tu au tuangazie na “nonsense” nyingine zote?
Hili ni bandiko lililotokana na makala yangu hii, kwenye Safu yangu ya “Kwa Maslahi ya Taifa”, kwenye gazeti la Nipashe kila siku za Jumapili. Kila nipatapo muda, huja na hizi makala zangu za “Kwa Maslahi ya Taifa” ambazo huja kwa mtindo wa swali, halafu jibu utatoa wewe msomaji mwenyewe.
Makala ya leo, ni makala ya pongezi kwa Rais Samia, kwa “nonsense” ya sukari, Rais Samia, anastahili pongezi za dhati, swali ni jee tuishie kwenye nonsense ya sukari tuu, au tuangazie na nonsense nyingine zote tuziache tusonge mbele? .
Naomba kuanza mada yangu ya leo, kwa kufundisha lugha kidogo, neno “nonsense” ni neno la kizungu lenye kumaanisha “ujinga”, hivyo uamuzi wowote unaoitwa “nonsense” ni “uamuzi wa kijinga”, Baba wa Taifa, alilitumia sana neno hili “nonsense”, ila yeye Baba wa Taifa, haikuishia tuu kwenye kulaumu maamuzi ya kijinga, “nonsense”, bali pia aliwaita watoa maamuzi hayo ni “wajinga”, ninanayo mifano mingi ya Mwalimu Nyerere kutumia neno “nonsense”
Mfano mzuri kabisa ni wakati Mwalimu Nyerere anaaga na kung’atuka kwenye urais, alikiri serikali yake imefanya makosa mengi tuu , akakiri kuna baadhi ya maamuzi yalikuwa ni “nonsense”, makosa, lakini pia akasema “kufanya kosa sii kosa, kosa kurudia kosa”.
Wakati tukijiandaa kwa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi, ile 1995, Mwalimu alizungumza na sisi waandishi wa habari, kwenye ukumbi wa Hoteli ya Kilimanjaro, na mimi nilikuwepo, akizungumzia ubinafsishaji wa benki ya NBC, Mwalimu akaishangaa serikali kukubali masherti ya nchi mabeberu, kuwa NBC ni li benki likubwa sana, lenye nguvu sana, lazima livunjwe, ndipo turuhusu ushindani wa mabenki, Mwalimu akauliza, NBC ina ukubwa gani?, “a mere NBC?!, this is “nonsense”.