Msikilize Mwana Diaspora Huyu. Asema Mazito na Ya Msingi Kuhusu Diaspora Watanzania
Katika kuelekea Kongamano la 4 la Diaspora, litakalofanyika Zanzibar tarehe 23 na 24 ya huu, naomba umsikilize kwa makini Mwana Diaspora huyu. Huyu ni Mmoja wa ma Diaspora wa Tanzania, Dr. Hildebrand Shayo, aliyesomea Tanzania tangu shule ya Msingi, sekondari, degree ya kwanza na masters amesomea UDSM, ndipo akaenda nchini Uingereza kufanya Ph.D, baada ya hapo, akafanya kazi Uingereza kwa miaka 10, kisha akaamua kurudi nyumbani. Msikilize hoja zake za msingi sana kuhusu Diaspora wa Tanzania.